MAISHA NINI
Maisha ni fumbo,
Fumbo lililo na ufiche,
Ufiche mgumu kufichuka,
Ukifichuka, mfichuzi hana woga wowote,
Woga huna nafasi kwa anayejua hatima yake.
Maisha ni ndoto,
Ndoto iliyoshamiri giza na nuru,
Giza ambayo mwanadamu hupapata ndani,
Nuru ambayo humjia mshindi wa giza,
Giza ndiyo njia ya nuru.
Maisha ni meli,
Meli iliyoanza safari,
Safari yenye mawimbi na misukosuko,
Mawimbi na misukosuko ndiyo humtaini mja,
Matokea ya mtihani hupa maisha mwelekeo.
Maisha ni nahodha,
Nahodha stadi huimarisha chombo chake,
Nahodha mwoga huyumbisha chombo chake,
Mawimbi na misukosuko humtaini nahodha,
Aliye bora hufikia ufuo salama.
Maisha ni riadha,
Riadha ya masafa marefu,
Kila mwanariadha huaza,
Lakini wachache ndio hutuzwa,
Watuzwao Ni wale walioniidhamisha miili yao.