Kwa nafsi yangu
Nafsi,
Nini lengo na ndoto yako,
Wapi hapo unataka nikupeleke,
Nini litakalo kurithisha nikupe,
Unataka nini, usinihangaishe.
Nafsi,
Kwa yote wengine hufanya sifanyi,
Sina nguvu Zaidi ya uwezo wako,
Yote nisiyofanya wewe hupedezwi,
Sababu unayoijua wewe mwenyewe.
Nafsi,
Wengi husema mambo huwa wazi,
Unapotazama nyuma si mbele,
Kumbuka vile tumetembea na tukawa pamoja,
Hujawai nitaliki nami pia sijawai kutaliki.
Nafsi,
Nikumbatie, niongoze, niadhibu,
Nami nitafikia,
Kilele utakacho,
Nitakurithisha ifaavyo.
Nafsi,
Ndani yangu ni mkusanyiko wa vizazi,
Wewe ndio mpatanishi ndani yangu,
Nipe amani, ushujaa, usawa, ukakamavu,
Hivyo sitawai kusaliti wewe.
Nafsi yangu,
Kwako mimi ni kitabu,
Umenisoma na umenielewa,
Sina cha siri,
Sina aibu mbele yako.