AFRIKA
Taifa langu,
Urithi wa waafrika,
Unayewanawirisha waafrika,
Tegemeo la watu weusi.
Taifa langu,
Wewe uliyedtaarabika wa kwanza,
Himaya za waafrika zilinawiri humu,
Kwa karne na karne ya miaka.
Taifa langu,
Unadhihirisha nafasi binadamu ulimwenguni,
Kupitia kwako mwanadamu amethibiti asili,
Mwanadamu amefuga wanyama na vyakula.
Taifa langu,
Wewe Ni nyota ya ulimwengu,
Omeonyesha amani inawezekana,
Wanadamu wanaweza kujiamulia hatima yao.
Taifa langu,
Wewe ni mfano wa kuigwa,
Huna silaha za uharibifu,
Binadamu kweli hahitaji mabomu ama nuklia.
Taifa langu,
Wanao wanakutazama,
Wape amani, Faraja na mafanikio.